Friday, January 22, 2016

Mshabiki maarufu wa Yanga maarufu kama "Ally Yanga" apata ajali.... SOMA HAPA kwa Maelezo zaidi....


Wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 5-0, magoli yaliofungwa na Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Amis Tambwe alieibuka shujaa kwenye mchezo huo baada ya kufunga goli tatu (hat-trick) na kuipeleka Yanga kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.


Hali si shwari kwa Mshabiki Mkubwa na maarufu wa Yanga ajulikanae kama "Ally Yanga" ambae katika safari yake ya kwenda kupumzika kwake huku akiwa na furaha ya Ushindi alipata ajali ya Pikipiki usiku wa kuamkia leo, na kukimbizwa hospitali. Hili ni pigo kwa wachezaji na mashabiki wenzake..

Mungu amsaidie..


No comments:

Post a Comment