Monday, February 1, 2016

PICHA ZIMA la Majangili waliotungua Ndege ya askari wa doria huko Maswa Shinyanga SOMA HAPA>>>

Kwa mara ya kwanza katika historia ya uhifadhi nchini majangili wa tembo wametungua chopa ya askari wa doria iliyokuwa ikimilikiwa na mwekezaji wa kitalu cha mwiba holdings katika pori la tengefu la maswa mkoani  wilayani meatu mkoani simiyu na kusababisha kifo cha rubani wa chopa hiyo huku rubani mwenzie akijeruhiwa vibaya mguuni Chopa hiyo inasemekana ilitunguliwa majira ya saa kumi na mbili jioni jana na Majaangili hao ambao wanaosadikika kutumia silaha nzito za kivita walifanikisha kutekeleza uhalifu huo walipo gundua kuwa chopa hiyo ilikuwa ikiwafuatilia baada ya kubaini mahali walipo na uhalifu waliokuwa wakiutekeleza katika pori hilo,ambapo inaripotiwa kwamba pamoja na kutungua chopa hiyo walisha fanikiwa kuuwa tembo watatu

Polisi nchini Tanzania wanasema kuwa wamewakamata washukiwa watatu wa mauaji ya rubani mmoja Muingereza aliyekuwa akisadia kupepeleza visa vya mauaji ya ndovu katika mbuga ya wanyama ya Maswa.

Rubani huyo Roger Gower aliaga dunia baada ya wawindaji haramu kumfyatulia risasi .
Msemaji wa shirika linalosimamia mbuga za wanyama nchini Tanzania Pascal Shelutete amesema kuwa mizoga tatu ya ndovu ilipatikana karibu na eneo la ajali dhihirisho kuwa aliyeishambulia helikopta hiyo alikuwa amejihami vilivyo na huenda alikuwa na shehena hiyo ya meno ya ndovu.

Msako bado unaendelea Kaskazini mwa Tanzania, kulitafuta kundi la majangili wanaouwa tembo, na ambalo lilimpiga risasi na kumuuwa rubani huyo kutoka Uingereza.
Roger Gower aliweza kutua ndege yake katika mbuga ya Maswa, baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa, lakini alikufa baadae kutokana na majaraha aliyopata.
Mbunge mmoja wa Tanzania, Lazaro Nyalandu, alilaani mauaji hayo na kusema kuwa ni waovu na waoga.


Shirika moja la wakfu wa utunzaji wa mazingira, ndilo lililotangaza kuwa rubani mmoja raia wa Uingereza, alikuwa amepigwa risasi na kuuawa kaskazini mwa Tanzania.


SOURCE:http://startvtz.com/ndege-ya-askari-wa-doria-yatunguliwa-na-majangili-shinyanga/
SOURCE: http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/01/160131_tanzania_pilot_shot

No comments:

Post a Comment