Saturday, January 16, 2016

DARASA LA ALAMA MBALIMBALI ZA MOBILE NETWORKS

Terminologies 2G, 3G, H, H+ au E etc, je maana yake ni nini kwenye network?
Ni speed zinazotumika kusafirisha data kwenye internet ambapo zinatofautiana uwezo kutokana na teknolojia:
1. Letter G stands for GPRS (General Packet Radio Service) na ndio first generation ya mobile phone
Hua inamaanisha spidi ya internet yako ni ndogo sana (86kbps)
technology.
2. Letter E stands for EDGE (Enhanced Data Rates for GSM evolution) hua inamaanisha speed ya internet yako ni ndogo ila ina afadhali kidogo kuliko G (236kbps)
3. Letter 2G (Second Generation) Ni generation ya pili ya mobile phone technology ambayo nayo inatumia GPRS system lakini speed yake ni kubwa kidogo than letter G, (154kbps) ila ni ndogo than letter E yaani ipo katikati ya G na E.
4. Letter 3G (Third Generation of mobile technology) Inatumia UMTS & imebase kwenye GSM system, na ina speed kubwa kuliko hizo (speed yake 386kbps)
5. Letter H stands for HSPA (High Speed Packet Access) Ni muendelezo baada ya 3G ambayo ina speed kubwa (like 3.2 Mbps)
6. Letter H+ stands for enhanced HSPA, Yaani hii ina speed kubwa zaidi ya H kama nilivyoielezea inauwezo wa kutransfer data up to 7.2 Mbps, ndio inayotumika kwenye simu nyingi nowadays.
7. Letter 4G (Fourth Generation of Mobile phone Technology) pia inajulikana kwa jina la LTE (Long Term Evolution).
Model hii ndio current kwa sasa ambayo inatumia H+, so itakuwa na speed kubwa zaidi (like 14.4mbps to 21mbps)
8. Letter WCDMA stands for Wide-band Code-division Multiple Access. Inatumia teknolojia ya 3G ila imeongezewa GSM ambayo inaiongezea speed ya kusafirisha data na ndiomaana simu nyingi zimeitumia kabla ya kuja kwa 4G.
So ukiona alama hizo kwenye simu yako maana yake ni kama nilivyozielezea hapo awali.

NB: Nimeongelea kuhusu kbps na Mbps maana yake ni:
Mbps:  maana yake ni Mega bits per second yani kiasi cha data kinachoweza kusafirishwa kwa sekunde kwenye internet.
Kbps:  maana yake ni kilobits per second, hii ni ndogo kuliko mbps.
i.e. 1 kbps = 0.001mbps
Nafikiri kila mtu atakuwa ameelewa hizo network symbols kwenye simu yake.
But sometime unaweza ukaona alama hizo zinabadilika badilika kwenye sim yako inakuwa ni kwasababu ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya internet
So internet signal ikiwa vizuri alama inabadilika to H hadi H+ na ikiwa low inashuka to 3G had 2G au G, kulingana na version ya simu.

Nafikiri sasa hutamlaumu aliyekuuzia simu kwa kusema haikai 3G, tatizo litakuwa ni la network au technology ya simu yako.

No comments:

Post a Comment