Monday, January 25, 2016

Bunge Jipya lanoga... Mitazamo tofauti yaibuka.. SOMA HAPA KUPATA MITAZAMO TOFAUTI ILIOTOLEWA MITAANI..

Kesho wabunge wanarudi bungeni kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni bunge jipya kabisa chini ya Spika Mheshimiwa Job Ndugai na Dk. Tulia, Wananchi wengi wakiwa na matizamo tofauti kuhusu bunge jipya kutokana na mabadiliko mbali mbali yaliyotokea ndani ya bunge hilo kutoka lililo pita.

Wengi wamekuwa na mitazamo tofauti wengi wakiwa wanamategemeo kuwa litakuwa na upinzani  mkubwa kutokana na upinzani kuongezeka maradufu, wengine wakipendekeza sheria dhidi ya wabunge na wazembe ziwekwe uzembe huo ulitajwa kuwa ni kulala, kushikana mashati na kujibizana matusi, huku wengine wakisema wanategemea kilekile maana wakina “hela ya Mboga ndio walewale wameingia” hii ni mitazamo tofauti iliotolewa vijiweni siku ya leo ikiwa ni njia mojawapo ya kupata maoni ya wananchi juu ya bunge jipya.

No comments:

Post a Comment