Wednesday, February 17, 2016

NECTA CSEE RESULT 2015.... PLEASE READ>>>

In the social media a lot of rumors were going on, basically on the actual date when CSEE 2015 will be out, different messages where sent with gossiping on the internal matters within the council as shown below,


BREAKING NEWS!!
Ofisi ya wizara ya elimu kupitia kwa waziri wa wizara hiyo ndugu JOYCE NDALICHAKA,imetangaza kuwa,matokeo ya kidato cha nne yamezuiliwa kwa muda kupisha uchunguzi,inadaiwa matokeo hayo yalifanyiwa uchakachuzi kwani wanafunzi wengi wamefeli kwa uzembe wa wasahihishaji,hivyo mitihani hiyo itasahihishwa tena na matokeo yatangazwa tena tarehe 08/03/2016.wasahihishaji wamekamatwa k
upisha uchunguzi.wizara inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.mara upatapo taarifa hii wataarifu na wenzio.



The information above is wrong according to the NECTA public relation officer as shown,

Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba  ufafanuzi kuhusu  taarifa  zinazosambazwa  kwenye  mitandao  ya kijamii kuwa Wizara  ya  Elimu,  Sayansi,  Teknolojia  na  Ufundi imetangaza kuwa  matokeo  ya  Mtihani  wa  Kidato  cha  Nne  (CSEE)  2015  yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016.Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla  kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki.Hivyo,Baraza  linaomba  umma  kuzipuuza  taarifa  hizo  kwa  kuwa Wizara haijasitisha utoaji  wa matokeo hayo, Matokeo yatatangazwa  mara tu mchakato utakapokamilika.
Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO



For more
http://www.necta.go.tz/files/TANGAZO%20MATOKEO%20CSEE2015%20two.pdf

No comments:

Post a Comment