Sunday, November 29, 2015

Mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo!!!

Wazazi wengi huwagombeza watoto wakikuwa kuwa wamebadilika na mara nyingi hawana heshima. Ni jambo la kawaida kwa familia nyingi wazazi huishia kujiuliza na kusingizia tabia mtoto katoa wapi, lakini tokana na uhalisia tabia yeyote anayoonyesha mtoto inatoka katika jamii imzungukayo.
Tutoke nje ya nchi kidogo tumwangalie Will Smith muigizaji mwenye asili ya kiafrika amerika (yaani black America) ambaye familia yake yote imedumbukia kwenye uigizaji.
Tukirudi Tanzania tunakutana na msanii hayati TX Moshi ambaye mwanae yupo kwenye tasnia ya sanaa ya kuigiza.
Je hawa walelewao wengine na wasanii wa kizazi hiki watakuwaje?, Je wataiga maisha ya baba zao? au watapata njia nyingine?


Saturday, November 28, 2015

Kukagua simu ya mwenza wako ni kujiumiza roho, Mwone Diamond akitafuta ugomvi kwa Zari.

Wapenzi wengi wana tabia za kuchunguza simu za wenzao,  hii ni sababu ya kukosa uaminifu. Hii tabia sio nzuri maana hupunguza uaminifu ndani ya mahusiano.
Msanii Diamond atangaza kutohusika na kuchunguza simu ya mpenzi wake Zari, lakini picha hii haionyeshi uuhalisia.

Sababu 10 zivunjazo ndoa nyingi... Vijana na Wanandoa soma hapaa....

1. upendo
Upendo wa kweli ni jambo muhimu sana katika maisha ya ndoa, vijana wengi hukimbilia ndoa kisa mali hasa vijana wa kike, bila kusahau ndoa ni pingu za maisha na huyo mtu utakaa nae milele. Upendo wa kweli usipokuwepo katika ndoa hii ndoa haiita dumu maana amani haita kuwepo pia faraja kati ka wanandoa haitopatikana na hio ndoa kugeuka maigizo.

2. uaminifu
Kama upendo wa kweli ukiwepo ndani ya nyumba, uaminifu hasa ndio waaitajika, kama hamta aminiana vitu vidogo tu vitawatenganisha, maana jamii kawaida huonea wivu ndoa na kutupa mishale ya maneno na matendo ili kuijeruhi ndoa yenu, na siri za ndani ni zenu kama wana ndoa sio za wote, na kama uaminifu hauta kuwepo ndoa itakaa kwa mashaka, na ndoa ya mashaka haidumu.

3. Msamaha
Kuna msemo wa kiingereza unasema “no body is perfect” kiswahili inamaana kuwa, “hakuna alie msafi” hii inamaanisha kuwa binadamu hukosema na anahitajika kusamehewa,kama ndoa haita weka msamaha kama ngao yao, muhimili wa ndoa hii uko matatani.

4.Uvumilivu
 Ndoa imeundwa na watu wawili ambao walitoka nyumba tofauti na maisha tofauti kabisa, ndoa huwajumlisha kutokana na tofauti zao, kabla ya ndoa kuna kitu kinachoitwa courtship(Uchumba) hiki ni kipindi ambacho wapenzi hujuliana tabia zao na kuunganisha tofauti zao na kawaida hutumia mwaka 1 mpaka 4 na ikizidi hapo ni tatizo, kukiruka au kukizidisha hiko kipindi huaribu ndoa nyingi sana na kama hapakuwa na maelewano ya tabia hapa mnaruhusiwa kuachana na kama ukilazimisa hiyo ndoa haitadumu.

5.Mawazo Mgando
Katika ndoa wanawake wengi huwategemea wanaume katika kutafuta, na hata wengine wakijiita ni wanawake wa nyumbani, pia kuna wanaume wanao lelewa, ndoa haiwezi endelea kama hapatakuwa na maendeleo maana mwaweza pata watoto na kipato toka uchumba hadi mna watoto watatu ni kile kile mwisho wa siku ndoa huvunjika kisa kipato shida, mwanandoa kutumia njia mbadala(wizi, uzinzi n.k), kwa mwanamke epuka kuwa mke wanyumbani na mwanaume atafute kazi, hii pia husaidia katika tendo maana wote mnakuwa mmechoka tendo mnafanya kutafuta usingizi, vinginevyo ndio mchepuko unapoanzia.

6. Mazoea
Mke ndio mpishi wa chakula cha ndoa, hata katika mapishi ya kawaida chakula huwa kina badilishwa tokana na ratiba au mpishi atavyojisikia, chakula cha ndoa kinaitaji maandalizi sawa na chakula cha tumbo, namaanisha kuwa mke na mume wanahitaji kujiandaa na kama hawatajiandaa hata  dakika 1 mwanaume hatafika yaani ataonja tu chakula cha ndoa na kulala, hii ni sawa na maisha ya kawaida ya nyumbani, nyumba inatakiwa iwe safi na ibadilishwe mipango kuondoa mazoea, pia chakula kinahitaji kubadilika sio sikukuu tu, na  wapenzi wabadilike hata pawe na out.

7.kutotambua wajibu
Katika jamii yetu tumelelewa tukitambua wajibu wetu kwa kila jinsia tokana malezi na tamaduni, mwanaume alete chakula mezani  na mwanamke apike, lakini maisha yana badilika na sio kila siku sawa, mfano mke anamimba na vyombo havijaoshwa na nguo hazijafuliwa mwanaume akijitolea sio mbaya , tutambue wajibu wetu ili pande fulani isilalamike maana pakitokea malalamiko ndio mwanzo wa ndoa kuvunjika.

8.utii
Tukishatambua wajibu wetu na utii hufuata, hili ni jambo muhimu katika ndoa, kama utii haupo ndoa na hata familia yote inaweza tengana, usemapo utii tunaanzia kutoka kwa mtoto mpaka kwa kichwa cha familia.

9. Uchafu
Hili ni tatizo kubwa sana ambalo huwezwa kufichwa katika kipindi cha uchumba, ila ni shida kulificha katika kipindi cha ndoa maana mko mwili mmoja, usafi unaoitajika ni wa mwili na roho, mwili unahusisha kuoga, kunawa miguu kabla ya kulala, sehemu za ndani za siri, harufu za makwapa, nakadhalika.Usafi uzingatiwe katika ndoa na wanandoa wajaribu kufanya usafi kuwa sehemu ya maisha yao maana kuna msemo usemao, “Ishi uongo mpaka uongo uwe maisha yako”.



10.kusahau uwepo wa Mungu

Uwepo wa Mungu katika ndoa hulinda tabia za wanadoa, ulinzi huu hufuatana na vitabu vya dini, ambavyo kazi zao ni kulinda maadili katika jamii, kusahau uwepo wa Mungu katika jamii huleta maovu ambayo husababisha mafarakano katika ndoa na hata kuvunjika kwake.

Saturday, November 21, 2015

Sababu za Mwanaume Kuchepuka, Jua akichepuka anamaanisha nini?

Tamaduni za kiafrika zimempa nguvu sana mwanaume katika maisha na jamii kwa ujumla, kitendo hiki kina mpa ujasiri na hata husababisha  kuweza na kutamani kujaribu vitu vingi tu ikiwa kama kuonja ladha ya mwanamke mwingine zaidi ya mpenzi wake ikiwa kama jaribio.
Hali hii inaonekana ni mazoea au ukaidi ila kwa mtazamo wangu ndio Mwanaume alivyoumbwa, ameumbwa akitamani chochote kizuri na kukichukua na ndio maana nirahisi yeye kupata maendeleo binafsi.
Tuchukulie mfano wa jogoo, anaweza pita kwa matetea wote wa jirani pale ambapo jogoo wa jirani ni mdhaifu na hawezi kutetea tetea walio mzunguka, sawa na wanaume, hupita na kudonyoa kwa wanaume wenziwe wasio linda malizao vizuri!, kama vile jogoo hatasahau nyumbani na kutoa chakula kwa kila tetea atakae mpita na mwanaume yuko vile vile(wanaita kuhongwa)...


Bila kusahau jogoo hurudi nyumbani jioni na kutunza wanawe alio waacha kwa mama yao siku nzima bila kujua wamekula nini, pia mwanaume ni sawa sawa maana hajui familia imekula nini bali huleta kidogo kilichobaki baada ya kula na michepuko huku akijisikitikia vingi alivyopoteza.
Maana ya kurudi mwishoni ni kudhirisha upendo mwanaume alionao kwa mwenzi wake ambao hakuupata huko alipopita, na asiporudi ujue upendo uliompa hauna mashiko.
Huyu mzee nuksi!!, hata akifanya yake tutasema anaigiza.