1. upendo
Upendo wa kweli ni jambo muhimu sana katika maisha ya ndoa, vijana wengi
hukimbilia ndoa kisa mali hasa vijana wa kike, bila kusahau ndoa ni pingu za
maisha na huyo mtu utakaa nae milele. Upendo wa kweli usipokuwepo katika ndoa
hii ndoa haiita dumu maana amani haita kuwepo pia faraja kati ka wanandoa haitopatikana
na hio ndoa kugeuka maigizo.
2. uaminifu
Kama upendo wa kweli ukiwepo ndani ya nyumba, uaminifu hasa ndio waaitajika,
kama hamta aminiana vitu vidogo tu vitawatenganisha, maana jamii kawaida huonea
wivu ndoa na kutupa mishale ya maneno na matendo ili kuijeruhi ndoa yenu, na siri za ndani ni zenu kama wana ndoa sio za wote, na kama
uaminifu hauta kuwepo ndoa itakaa kwa mashaka, na ndoa ya mashaka haidumu.
3. Msamaha
Kuna msemo wa kiingereza unasema “no body is perfect” kiswahili inamaana
kuwa, “hakuna alie msafi” hii inamaanisha kuwa binadamu hukosema na anahitajika
kusamehewa,kama ndoa haita weka msamaha kama ngao yao, muhimili wa ndoa hii uko
matatani.
4.Uvumilivu
Ndoa imeundwa na watu wawili ambao
walitoka nyumba tofauti na maisha tofauti kabisa, ndoa huwajumlisha kutokana na
tofauti zao, kabla ya ndoa kuna kitu kinachoitwa courtship(Uchumba) hiki ni
kipindi ambacho wapenzi hujuliana tabia zao na kuunganisha tofauti zao na
kawaida hutumia mwaka 1 mpaka 4 na ikizidi hapo ni tatizo, kukiruka au
kukizidisha hiko kipindi huaribu ndoa nyingi sana na kama hapakuwa na maelewano
ya tabia hapa mnaruhusiwa kuachana na kama ukilazimisa hiyo ndoa haitadumu.
5.Mawazo Mgando
Katika ndoa wanawake wengi huwategemea wanaume katika kutafuta, na hata
wengine wakijiita ni wanawake wa nyumbani, pia kuna wanaume wanao lelewa, ndoa
haiwezi endelea kama hapatakuwa na maendeleo maana mwaweza pata watoto na
kipato toka uchumba hadi mna watoto watatu ni kile kile mwisho wa siku ndoa huvunjika
kisa kipato shida, mwanandoa kutumia njia mbadala(wizi, uzinzi n.k), kwa
mwanamke epuka kuwa mke wanyumbani na mwanaume atafute kazi, hii pia husaidia
katika tendo maana wote mnakuwa mmechoka tendo mnafanya kutafuta usingizi,
vinginevyo ndio mchepuko unapoanzia.
6. Mazoea
Mke ndio mpishi wa chakula cha ndoa, hata katika mapishi ya kawaida chakula
huwa kina badilishwa tokana na ratiba au mpishi atavyojisikia, chakula cha ndoa
kinaitaji maandalizi sawa na chakula cha tumbo, namaanisha kuwa mke na mume
wanahitaji kujiandaa na kama hawatajiandaa hata
dakika 1 mwanaume hatafika yaani ataonja tu chakula cha ndoa na kulala,
hii ni sawa na maisha ya kawaida ya nyumbani, nyumba inatakiwa iwe safi na
ibadilishwe mipango kuondoa mazoea, pia chakula kinahitaji kubadilika sio
sikukuu tu, na wapenzi wabadilike hata
pawe na out.
7.kutotambua wajibu
Katika jamii yetu tumelelewa tukitambua wajibu wetu kwa kila jinsia tokana
malezi na tamaduni, mwanaume alete chakula mezani na mwanamke apike, lakini maisha yana
badilika na sio kila siku sawa, mfano mke anamimba na vyombo havijaoshwa na
nguo hazijafuliwa mwanaume akijitolea sio mbaya , tutambue wajibu wetu ili
pande fulani isilalamike maana pakitokea malalamiko ndio mwanzo wa ndoa
kuvunjika.
8.utii
Tukishatambua wajibu wetu na utii hufuata, hili ni jambo muhimu katika ndoa,
kama utii haupo ndoa na hata familia yote inaweza tengana, usemapo utii tunaanzia
kutoka kwa mtoto mpaka kwa kichwa cha familia.
9. Uchafu
Hili ni tatizo kubwa sana ambalo huwezwa kufichwa katika kipindi cha
uchumba, ila ni shida kulificha katika kipindi cha ndoa maana mko mwili mmoja,
usafi unaoitajika ni wa mwili na roho, mwili unahusisha kuoga, kunawa miguu
kabla ya kulala, sehemu za ndani za siri, harufu za makwapa, nakadhalika.Usafi
uzingatiwe katika ndoa na wanandoa wajaribu kufanya usafi kuwa sehemu ya maisha
yao maana kuna msemo usemao, “Ishi uongo mpaka uongo uwe maisha yako”.
10.kusahau uwepo wa Mungu
Uwepo wa Mungu katika ndoa hulinda tabia za wanadoa, ulinzi huu hufuatana na
vitabu vya dini, ambavyo kazi zao ni kulinda maadili katika jamii, kusahau
uwepo wa Mungu katika jamii huleta maovu ambayo husababisha mafarakano katika
ndoa na hata kuvunjika kwake.