Wednesday, December 9, 2015

Uhuru day yageuka Usafi Day... Waziri Mkuu Bwana Kassim Majaliwa aitembelea K/koo...

Katika hali inayo staajabisha, Waziri mkuu wa Jamhuri ya Tanzania ameoneka Kariakoo jijini Dar es salaam ambapo watu walimpokea kwa shangwe na kazi za usafi ikiwa ni moja kati ya tekelezo la raisi wa awamu ya tano Bwana John Pombe Magufuli.

Wakazi wa Kariakoo walifarijika na kutembelewa na Waziri Mkuu huyo ktokana na viongozi wengi kutokumbuka sehemu hizo na wakiwaliamua kumuunga mkono waziri mkuu wa Tanzania huku wakisindikiza kwa nyimbo na shangwe ikiwemo sehemu  ilionukuliwa kuwa "Mafisadi wataisoma namba", huku wengine wakisema,"Tumbueni Majipu, chunusi mpaka manundu".

Sehemu mbalimbali za Dar es salaam zimeonekana zikifanyiwa usafi, hii ikijumuisha usafi wa majumbuni na Masokoni mfano mzuri umeoneshwa katika soko maarufu la Mbuzi vingunguti ambapo uchafu ulizoeleka sana, sasa limependeza na usafi bado kuendelea.

No comments:

Post a Comment