Sunday, December 6, 2015

JINSI YA KUWEKA LENGO NA KUFANIKISHA

KWANINI TUNAWEKA MALENGO?
1. Tunaweka malengo kwasababu ni kitu sahihicha  kufanya, ni sawa na kucheza mpira bila nguzo za goli au viashiria vya sehemu ya kufunga haita kuwa na maana sahihi ya mchezo.

2. Kuweka malengo husaidia katika kujiweka imara kufikia mafanikio katika shughuli zako.

3. Kuweka malengo hukusaidia kujenga nidhamu sahihi kuelekea mafanikio yako.

4. Kuweka malengo hukusaidia kujua maendeleo ya shughuli zako, pia ni njia ya kupima mafanikio katika muda fulani.

5.Kutokuwepo na lengo ni sawa na kutokuwa na upeo na mipango katika shughuli zako.

JINSI YA KUWEKA NA KUYAFIKIA MALENGO

1. Andika Lengo Wanasema mali bila daftari hupotea bila habari, lengo ni mali yako usipoiandika hupotea kama ndoto, na kuandika huleta uhalisia wa malengo yako.

2.Andaa Lengo
Lengo huitaji maandalizi thabiti ili liwe uhalisia, bila maandalizi thabiti lengo huwa kama ndoto nyingine yaani hupotea na kukuachia kumbukumbu,japo kama umefika sehemu ya maandalizi waweza pata hata hasara, maandalizi yaweza chukua hata miaka miwili lakini yasizidi hapo.

3. Fanya Lengo
Lengo linaweza kuwa kubwa lakini ukianza hata kufanya kidogo kidogo husaidia na kukufariji maana umefanya jambo muhimu kuanza, na kushaanza usitegee matokeo ya papo kwa hapo, hakuna kitu chenye malipo ya sekunde hiyo hiyo, hata dawa huchelewa kufanya kazi hata kama inaponyesha.

4. Fanikisha Lengo
Baada ya kufanya shunguli uliopanga kidogo kama kianzio, huu ni muda wa kutimiza lengo kamili. Unaweza kuwa ni wakati mgumu  sana lakini ukijiamini na kutumia malighafi zote zilizokuzunguka kama watu, ardhi nakadhalika linaweza fanyikiwa.

5.Dumisha Lengo
Lengo linatakiwa lidumu ili isionekane kama umeshindwa kuendeleza lengo lako, muda wa kudumu lengo lililo pangwa hutengemea na jinsi ulivyoliandaa lengo lako litumike muda gani.

6.Kuza Lengo
Lengo lako kama limeandaliwa kaajili ya watu au sehemu Fulani linatakiwa likuzwe ili lisaidie wengi, na hii huitaji gharama na kujipanga ila huwezekana sana tu.

7.Shirikisha Lengo
Kishirikishana ni upendo, na jinsi unavyoshirikisha wengine ndio jinsi unavyopata mawazo mapya juu ya malengo yako, lakini angalia unavyoshirikisha maana sa nyingine wengine huvunja moyo.


Ni wakati wa mafanikio SHARE kama unahisi imekusaidia.

No comments:

Post a Comment