
Saturday, January 30, 2016
Gumzo mitandaoni>>>> Rais wa marekani barak Obama Kukimbia kuwahi ndege yake baada ya kutumia muda wake vibaya....

Monday, January 25, 2016
SPIKA WA BUNGE AREJEA KUTOKA INDIA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai amerejea kutoka nchini India alikokuwa akifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Mhe. Ndugai pia amewashukuru watanzania wote kwa dua na sala zao katika kipindi alichokuwa India ambazo zimemuwezesha kuimarika kwa afya yake na hatimaye kurejea nchini salama.
Mbali na kutoa shukrani hizo Mheshimiwa Ndugai pia amewatakia Watanzania wote kheri na nafaka ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Sambamba na hilo Mhe Ndugai amewakumbusha pia Waheshimiwa Wabunge kujiandaa na shughuli za Bunge ambazo zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Mhe. Ndugai alilakiwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson ambaye aliambatana na Viongozi wengine wa kitaifa akiwemo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Merdad Kaleman, Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura, Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema na Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah.
SOURCE: http://www.parliament.go.tz/news/spika-wa-bunge-arejea-kutoka-india
Bunge Jipya lanoga... Mitazamo tofauti yaibuka.. SOMA HAPA KUPATA MITAZAMO TOFAUTI ILIOTOLEWA MITAANI..
Wengi wamekuwa na mitazamo tofauti wengi wakiwa
wanamategemeo kuwa litakuwa na upinzani
mkubwa kutokana na upinzani kuongezeka maradufu, wengine wakipendekeza sheria
dhidi ya wabunge na wazembe ziwekwe uzembe huo ulitajwa kuwa ni kulala, kushikana
mashati na kujibizana matusi, huku wengine wakisema wanategemea kilekile maana
wakina “hela ya Mboga ndio walewale wameingia” hii ni mitazamo tofauti
iliotolewa vijiweni siku ya leo ikiwa ni njia mojawapo ya kupata maoni ya
wananchi juu ya bunge jipya.
Sunday, January 24, 2016
Hotuba ya Raisi John Pombe Magufuli.... KUIPATA YOTE SOMA HAPA>>>>>>
Hotuba ya Raisi John Pombe Magufuli bado Kitendawili....

Labda tunaishi kwa Mazoea ya Raisi mstaafu, na inaweza kuwa ni sahihi Raisi kuto hutubia wananchi kwa zaidi ya kipindi cha miezi miwili lakini ni muhimu wananchi kujua mipango ya Raisi katika serikali na kuangalia matazamio ya baadae. Huu ni ushauri wangu(Kubwa lao) kuwa Raisi ajipange na atoe hotuba tujue mikakati tunayotakiwa kuiunga mkono, inaweza isiwe kila mwezi ila hata baada ya miezi mitatu itapendeza maana si sahihi kila mwezi hotuba itolewe bila kufanyika chochote.
Ni Mtazamo tu...
Saturday, January 23, 2016
Simu ya Raisi yawa gumzo mitandaoni..... Wengi wahusisha na utani wa lile kabilaa... Unajua ni lipi...

Hii imepelekea kumuhusisha na utani wa makabila, pia utumiaji wake wasimu na kushona nguo pina nao umehusika. Utani huu sio kwa dharau na kejeli ila ni utani wa kujenga na kuonyesha upendo kwa raisi wetu baada ya kutuonyesha kuwa hajajilimbikizia.
kaza Buti Raisi wetu.
Hapa kazi tu...
Subscribe to:
Posts (Atom)