Tuesday, February 2, 2016

WHO yahofu virusi vya Zika kusambaa kwa kasi... JUA YOTE KUHUSU UGONJWA HATARI WA ZIKA, SOMA HAPA>>>>

Wataalam wa maswala ya afya wa shirika la Afya duniani WHO wanahofu kuwa virusi vinasambaa mbali na kwa haraka,vikisababisha madhara makubwa. Virusi hivyo vinavyosambazwa na Mbu, kama Dengue na vingine maambukizi yake yamekuwa yakihusishwa na maelfu ya watoto wanaozaliwa wakiwa na vichwa vidogo.
tahadhari ya WHO kuhusu Zika ni ya hali ya juu sawa na ya Ebola
hii inamaanisha kuwa utafiti na msaada itatolewa kwa haraka kupambana na maambukizi.
Mkurugenzi mkuu wa WHO, Margaret Chan amesema nguvu ya pamoja inahitajika kupambana na virusi hivyo
amesema masuala yanayopewa kipaumbele ni kuwalinda wanawake wajawazito na Watoto dhidi ya mbu wanaosambaza virusi.

Tangu mwezi Oktoba kumekuwa na ripoti ya kesi 4,000 za watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo nchini Brazil pekee.


Shirika la Afya Duniani (WHO) leo linafanya mkutano wa dharura kujadili kuenea kwa virusi vya Zika.
Mkutano huo mjini Geneva utajadili iwapo mlipuko wa virusi hivyo unafaa kutangazwa kuwa “dharura ya kimataifa”.
Maafisa wa WHO wamesema mlipuko huo wa Zika unabadilika utoka “hatari ndogo hadi kuwa wa hatari kubwa”.

Katika visa vingi, watu walioambukizwa virusi hivyo vya Zika huwa hawaonyeshi dalili zozote, lakini virusi hivyo vinadaiwa kusababisha maelfu ya watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo Amerika Kusini.


Kutangazwa kwa mlipuko wa sasa wa Zika kuwa “dharura ya kimataifa ya afya ya umma” kutavifanya virusi hivyo kutambuliwa kama hatari kubwa duniani na kupelekea pesa, rasilimali na wataalamu wa kisayansi kutengwa kuangazia tatizo hilo Amerika Kusini na katika maabara kote duniani.
WHO inaangazia sana hasa baada ya kukosolewa kutokana na ilivyoshughulikia mlipuko wa maradhi ya Ebola Afrika Magharibi.
  •     Kundi laomba wenye Zika waruhusiwe kutoa mimba
  •  “  Msishike mimba sasa”, mataifa yashauri wanawake


Wengi walisema ilichelewa sana katika kuchukua hatua, na huenda hilo lilichangia vifo vingi.


mbu aina ya Aedes aegypti

Katika mkutano huo wa leo, wataalamu wa kudhibiti magonjwa, wataalamu kuhusu virusi na wale wanaoangazia kutengenezwa kwa chanjo, watamfahamisha mkugugenzi mkuu wa WHO Dkt Margaret Chan habari muhimu kuhusu mlipuko wa Zika.
Wiki iliyopita, alisema: “ Kiwango cha wasiwasi ni cha hali ya juu, na pia hali ya suitafahamu.
“Kuna maswali mengi, na tunahitaji majibu upesi.”




SOURCE:http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/02/160201_zika_who


1 comment:

  1. Borgata Hotel Casino & Spa to Host Job Fair & Dinner
    BORGATA 영주 출장샵 HOTEL CASINO & SPA in Atlantic 충주 출장샵 City, NJ. 청주 출장샵 Get 제주 출장안마 the job fair & dinner experience 경상남도 출장안마 at Borgata Hotel Casino & Spa.

    ReplyDelete