KWANINI
TUNAWEKA MALENGO?
1. Tunaweka malengo kwasababu ni kitu sahihicha
kufanya, ni sawa na kucheza mpira bila nguzo za goli au viashiria vya
sehemu ya kufunga haita kuwa na maana sahihi ya mchezo.
2. Kuweka
malengo husaidia katika kujiweka imara kufikia mafanikio katika shughuli zako.
3. Kuweka
malengo hukusaidia kujenga nidhamu sahihi kuelekea mafanikio yako.
4. Kuweka
malengo hukusaidia kujua maendeleo ya shughuli zako, pia ni njia ya kupima
mafanikio katika muda fulani.
5.Kutokuwepo
na lengo ni sawa na kutokuwa na upeo na mipango katika shughuli zako.
JINSI YA
KUWEKA NA KUYAFIKIA MALENGO
1. Andika
Lengo
Wanasema mali bila daftari hupotea bila habari, lengo ni mali yako usipoiandika
hupotea kama ndoto, na kuandika huleta uhalisia wa malengo yako.
2.Andaa
Lengo
Lengo
huitaji maandalizi thabiti ili liwe uhalisia, bila maandalizi thabiti lengo
huwa kama ndoto nyingine yaani hupotea na kukuachia kumbukumbu,japo kama
umefika sehemu ya maandalizi waweza pata hata hasara, maandalizi yaweza chukua
hata miaka miwili lakini yasizidi hapo.
3. Fanya
Lengo
Lengo
linaweza kuwa kubwa lakini ukianza hata kufanya kidogo kidogo husaidia na
kukufariji maana umefanya jambo muhimu kuanza, na kushaanza usitegee matokeo ya
papo kwa hapo, hakuna kitu chenye malipo ya sekunde hiyo hiyo, hata dawa
huchelewa kufanya kazi hata kama inaponyesha.
4.
Fanikisha Lengo
Baada ya
kufanya shunguli uliopanga kidogo kama kianzio, huu ni muda wa kutimiza lengo
kamili. Unaweza kuwa ni wakati mgumu
sana lakini ukijiamini na kutumia malighafi zote zilizokuzunguka kama
watu, ardhi nakadhalika linaweza fanyikiwa.
5.Dumisha
Lengo
Lengo
linatakiwa lidumu ili isionekane kama umeshindwa kuendeleza lengo lako, muda wa
kudumu lengo lililo pangwa hutengemea na jinsi ulivyoliandaa lengo lako
litumike muda gani.
6.Kuza
Lengo
Lengo lako
kama limeandaliwa kaajili ya watu au sehemu Fulani linatakiwa likuzwe ili
lisaidie wengi, na hii huitaji gharama na kujipanga ila huwezekana sana tu.
7.Shirikisha
Lengo
Kishirikishana
ni upendo, na jinsi unavyoshirikisha wengine ndio jinsi unavyopata mawazo mapya
juu ya malengo yako, lakini angalia unavyoshirikisha maana sa nyingine wengine
huvunja moyo.
Ni wakati
wa mafanikio SHARE kama unahisi imekusaidia.
No comments:
Post a Comment