Hotuba ya Raisi John Pombe Magufuli bado Kitendawili....
Sasa yapata zaidi ya miezi miwili tokea Raisi wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuapishwa kuwa Eaisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi wa Tanzania wamekuwa wakifuatilia kwa makini uongozi mpya huku wakiunga mikono jitihada mbalimbali zinazofanywa na viongozi wetu katika kuinuaa jamii yetu, na huku wengine kama sisi tukisubiri kwa hamu hotuba ya raisi wetu, huku tukitegemea itapagwa kama hotuba ile ya Bunge au zaidi.
Labda tunaishi kwa Mazoea ya Raisi mstaafu, na inaweza kuwa ni sahihi Raisi kuto hutubia wananchi kwa zaidi ya kipindi cha miezi miwili lakini ni muhimu wananchi kujua mipango ya Raisi katika serikali na kuangalia matazamio ya baadae. Huu ni ushauri wangu(Kubwa lao) kuwa Raisi ajipange na atoe hotuba tujue mikakati tunayotakiwa kuiunga mkono, inaweza isiwe kila mwezi ila hata baada ya miezi mitatu itapendeza maana si sahihi kila mwezi hotuba itolewe bila kufanyika chochote.
Ni Mtazamo tu...
No comments:
Post a Comment