Tamaduni za kiafrika zimempa nguvu sana mwanaume katika maisha na jamii kwa
ujumla, kitendo hiki kina mpa ujasiri na hata husababisha kuweza na kutamani kujaribu vitu vingi tu ikiwa
kama kuonja ladha ya mwanamke mwingine zaidi ya mpenzi wake ikiwa kama jaribio.
Hali hii inaonekana ni mazoea au ukaidi ila kwa mtazamo wangu ndio Mwanaume
alivyoumbwa, ameumbwa akitamani chochote kizuri na kukichukua na ndio maana nirahisi
yeye kupata maendeleo binafsi.
Tuchukulie mfano wa jogoo, anaweza pita kwa matetea wote wa jirani pale
ambapo jogoo wa jirani ni mdhaifu na hawezi kutetea tetea walio mzunguka, sawa
na wanaume, hupita na kudonyoa kwa wanaume wenziwe wasio linda malizao vizuri!,
kama vile jogoo hatasahau nyumbani na kutoa chakula kwa kila tetea atakae mpita
na mwanaume yuko vile vile(wanaita kuhongwa)...
Bila kusahau jogoo hurudi nyumbani jioni na kutunza wanawe alio waacha kwa
mama yao siku nzima bila kujua wamekula nini, pia mwanaume ni sawa sawa maana
hajui familia imekula nini bali huleta kidogo kilichobaki baada ya kula na
michepuko huku akijisikitikia vingi alivyopoteza.
Maana ya kurudi mwishoni ni kudhirisha upendo mwanaume alionao kwa mwenzi wake
ambao hakuupata huko alipopita, na asiporudi ujue upendo uliompa hauna mashiko.
Huyu mzee nuksi!!, hata akifanya yake tutasema anaigiza. |
No comments:
Post a Comment